Connect with us

Joto la mchezo wa wapoinzani wa jadi katika Soka la Tanzania, Simba na Yanga limefika nyuzi 90 huku dakika 90 zikisubirwa kuamua nani ataibuka mbabe.

Hata hivyo wakati mashabiki wengi wa soka wakijiuliza maswali mengi wachezaji Emanuel Okwi wa Simba na Obrey Chirwa wa Yanga ndio wanaotajwa sana na mashabiki wa soka kuwa huenda wakmaizeba timu zao katika mchezo huo.

Okwi tayari ameifungia Simba mabao 19 na kuwa kinara wa ufungaji wakati Chirwa ameifungia Yanga mabao 12 akiwa mfungaji anayeongoza katika klabu hiyo.

Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema Okwi ni mchezaji msikivu na anayejua kazi anayoifanya awapo uwanjani.

“Asingeweza kufanya mambo mazuri bila ushirikiano wa wachezaji wenzake, hata Bocco anafanya vizuri, ninawaamini wachezaji wangu na naamini watanipa matokeo mazuri,”amesema kocha huyo raia wa Ufaransa.

Hata hivyo walinzi wa Simba watapaswa kuwa makini na Chirwa pamoja na Ibrahim Ajibu ambao wanaweza kuleta madhara katika kikosi chao.

Katika mitaa mbali ya jiji mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wamekuwa wakitambiana kwa kuwataja wachezaji hao kuwa wataamua matokeo ya mchezo.

“Hatuna wasiwasi, Mnyama anakufa mapemaa si unamuona Chirwa pale mbele,’alisikika shabiki mmoja wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina la Said katika maeneo ya Tazara.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa