Connect with us

 

Mahakama Kuu nchini Kenya, imefutilia mbali uamuzi wa Shirikisho la soka FKF kumfungia rais wa zamani wa Shirikisho hilo FKF Sam Nyamweya miaka 10 ya kutojihusisha na maswala ya soka.

Aidha, Mahakama imewataka viongozi wa soka nchini humo kuacha kabisa kumzungumzia Nyamweya, na maswala yaliyojiri wakati wa uongozi wake.

Nyamweya alikwenda Mahakamani kupinga adhabu hii kwa madai kuwa inakwenda kinyume na haki zake kwa mujibu wa Katiba ya Kenya.

Kiongozi huyo wa zamani amekuwa akisema amestaafu uongozi wa soka, na hatua ya kufungiwa ni ya kushangaza.

Hata hivyo FKF, inasema ilichukua hatua hiyo baada ya kumpata Nyaweya na kosa la kufuja fedha za Shirikisho hilo, madai ambayo ameyakanusha vikali.

Kesi kati ya FKF na Nyamweya itaendelea mwezi Julai.

More in