Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Klabu ya Majimaji ya Songea imeafikiana kuvunja mkataba na mchezaji wake Abdulhalim Humud.

Mkataba huo umevunjwa baada ya pande mbili kukubaliana.

Akizungumzia hatua hiyo Humud alisema anataka kupata changamoto kwingineko.

“Mpira una mmbo mengi na sahizi tumekuwa watu wazima, nimeona nitafute nafasi kwingine,”alisema.

Humud amezichezea klabu mbalimbalj hapa nchini ikiwemo Simba, Mtibwa Sugar, Azam , Coastal Unioni na Cosmo ya Afrika Kusini.

Pia ameichezea Taifa Stars ambapo alikuwemo kwenye kikosi kilichocheza na Ivory Coast na Brazil mwaka 2010.

More in