Connect with us

Mchuano wa ufunguzi wa michuano ya soka ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani, utaanza kutifua vumbi kati ya wenyeji Morocco na Mauritania.

Mchuano huu, utachezwa katika uwanja wa Mohammed wa tano, mjini Casablanca kuanzia saa nne na nusu usiku saa za Afrika Mashariki Jumamosi usiku.

Hii ni mara ya nne tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009. Mwaka 2014, Morrocco ilifika katika hatua ya robo fainali ya michuano hii.

Mauritania nayo inacheza kwa tatu sasam mwisho ilikuwa ni mwaka 2014.

Refarii wa mchuano huu wa ufunguzi ni Janny Sikazwe kutoka nchini Zambia. Ni refa mwenye uzoefu mkubwa, amechezesha mechi kadhaa za Kimataifa.

Ratiba ya michuano ya ufunguzi:-

DRC imeshinda mara mbilli mwaka 2009 na 2016, Tunisia mwaka 2011.

Kundi A: Morocco, Guinea, Sudan na Mauritania

Januari 13 2018:- Morocco v Mauritania

Januari 14 2018:-Guinea v Sudan

Kundi B: Ivory Coast, Zambia, Uganda na Namibia

Januari 14 2018:-Ivory Coast v Namibia

Januari 14 2018:-Zambia v Uganda

Kundi C: Libya (Bingwa 2014) ,Nigeria, Rwanda na Equitorial Guinea

Januari 15 2018: Libya v Equitorial Guinea

Januari 15 2018: Nigeria v Rwanda

Kundi D: Angola, Cameroon, Congo na Burkina Faso

Januari 16 2018: Angola v Burkina Faso

Januari 16 2018: Cameroon v Congo

More in