Connect with us

Viongozi wa mataifa ya Amerika Kaskazini wametoa wito kwa wapiga kura, kutotilia maanani masuala ya siasa katika nchi hizo kuelekea upigaji kura kuamua iwapo Marekani, Canada na Mexico kuwa wenyeji wa kombe la dunia katika mchezo wa kandanda mwaka 2026.

Uamuzi huo utafanywa mwezi ujao jijini Moscow na marais wa vyama vya soka duniani nchini Urusi, kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Marekani Carlos Cordeiro, akizungumza na wanahabari wa michezo jijini Brussels, amesema iwapo mataifa hayo yatapata nafasi hiyo, Shirikisho la soka duniani FIFA litapata faida ya Dola Bilioni 11, toka Dola Bilioni 2.6 iliyopata nchini Brazil mwaka 2016.

Marekani, Canada na Mexico, zinapambana na Morocco kuwania nafasi hiyo ya kihistoria.

Morocco nayo imeendelea kuomba kura, huku mataifa ya Afrika na yale ya bara Asia yakisema yaliiunga mkono, wakati wa Uchaguzi huo tarehe 13 mwezi Juni.

More in