Connect with us

Mashabiki  17 wa soka wamepoteza maisha baada ya kukanyagana katika uwanja wa michezo wa Uige Kaskazini mwa nchi ya Angola.

Mashabiki wengine   zaidi ya mia moja wamejeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali mbalimbali nchini humo.

Ajali hii ilitokea wakati mashabiki hao wa soka walipokuwa wanasukuma kuingia uwanjani kutazama mchuano wa ligi kuu kati ya Santa Rita de Cassia na Recreativo do Libolo.

 Mashabiki hao walijaribu kuingia uwanjani licha ya uwanja huo kuwa umejaa na mkanyagano huo ulisababisha wengi kukosa hewa na kuzimia.

Mkasa kama huu uliwahi kushuhudiwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast baada ya watu 19 kupoteza maisha kukanyagana jijini Abidjan wakati wa mchuano kati ya timu ya nyumbani na Malawi.

Jijini Accra nchini Ghana, hali ilikuwa kama hiyo na kusababisha watu 127 kupoteza maisha.

More in