Connect with us

Jumapili na Jumapili wiki hii, kutakuwa na michuano kadhaa ya soka, hatua ya makundi, kutafuta nafasi ya kufuzu fainali ya bara Afrika mwaka 2019  nchini Cameroon.

Nchini Kenya, Harambee Stars itakuwa nyumbani kucheza na Black Stars ya Ghana, katika mechi ya kundi F.

Mechi hii itachezwa katika uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Kenya itakuwa bila ya nahodha wake wa siku nyingi Victor Wanyama anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Tottenham Hotspurs nchini Uingereza kwa sababu anauguza jeraha.

Nchini Uganda, the Cranes watakuwa wenyeji wa Taifa Stars ya Tanzania katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

Tanzania inakwenda katika mchuano huu wa kundi L wakiwa na kocha mpya Emmanuel Amunike, na wengi wanasubiri kuona kibarua chake cha kwanza kuona kitaanzaje.

Jijini Libreville, wenyeji Gabon watawakaribisha Burundi huku mabingwa watetezi Cameroon wakiwa mjini Moroni kucheza na Comoros.

Mechi zingine kesho:- Ushelisheli vs Nigeria, Namibia dhidi ya Zambia, Equitorial Guinea vs Sudan na Misri dhidi ya Niger.

Siku ya Jumapili, Rwanda itakuwa jijini Kigali kucheza na Cote Dvoire, Liberia itakuwa wenyeji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, huku Sudan Kusini wakicheza na Mali.

Hii ni michuano ya mzunguko wa pili, na michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini. Mshindi wa kwanza na wa pili, baada ya kumalizika kwa mechi za hatua ya makundi, atafuzu katika fainali hiyo.

More in Africa Cup of Nations