Connect with us

Mechi za mzunguko wa mwisho kuwania nafasi kucheza fainali ya soka kwa mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake, inachezwa siku ya Jumatano.

Fainali ya mwaka huu, itakuwa ya 11 tangu kuanza kwa mashindano haya 1998 yanayoandaliwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kila baada ya miaka miwili.

Ghana itakuwa mwenyeji wa mashindano haya, yatakayokutanisha mataifa nane katika michuano itakayochezwa kati ya tarehe 17 Novemba na tarehe 1 mwezi Desemba.

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili.

Mechi za kufuzu zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi, ataungana na wenyeji Ghana.

Ratiba:

Algeria vs Ethiopia

Ivory Coast vs Mali

Gambia vs Nigeria

Congo vs Cameroon

Kenya vs Equitorial Guinea

Lesotho vs Afrika Kusini

Zambia vs Zimbabwe

Mechi za marudiano ni wiki ijayo.

More in Africa Cup of Nations