Connect with us

Matokeo mabaya yamfukuzisha kazi kocha wa Thika United

Matokeo mabaya yamfukuzisha kazi kocha wa Thika United

Na Victor Abuso,

Kocha wa klabu ya soka ya Thika United nchini Kenya Tim Bryett amejiuzulu baada ya matokeo mabaya ya kuwania ubingwa wa ligi kuu mwishoni mwa juma lililopita.

Wakati Bryett akitangaza kujiuzulu kwake, aliwaambia uongozi wa Thika United kuimarisha uwanja wake wa nyumbani unaotumiwa na wachezaji wa klabu hiyo lakini pia kubadilisha sera ya kuwatumia wachezaji chipukizi na kufikiria kuwasajili wale wenye uzoefu.

Bryett ambaye alipewa kibarua cha kuifunza Thika United mwezi Januari mwaka huu ameicha klabu hiyo ikiwa na alama 25 na katika nafasi ya 11.

Naye naibu kocha wa AFC Leopards Yusuf Chipo alijizulu baada ya matokeo mabaya ya klabu hiyo hususan baada ya kufungwa na Ulinzi Stars bao 1 kwa 0 hivi karibuni.

Kocha wa Leopards ambayo ipo katika nafasi ya tano kwa alama 35 Zdravko Logarusic amerejea katika kikosi hicho baada ya kumaliza mgomo kwa sababu za kutolipwa marupurupu yake.

Leapards ipo katika nafasi ya tano kwa alama 35 wakati huu inapojiandaa kumenyana na Gor Mahia ambao ni watani wao wa jadi mwishoni mwa juma hili.

Nafasi ya kwanza inashikiliwa na mabingwa watetezi Gor Mahia ambao wana michuano miwili kibindoni na tayari wana alama 55 mbele ya wanajeshi Ulinzi Stars ambao wana alama 44 baada ya mechi 23.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in