Connect with us

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Salum Mayanga Alhamis Machi 8, 2018 saa 4 asubuhi atazungumza na Waandishi wa Habari za Michezo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF,Karume,Ilala,Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine kocha Mayanga pia atazungumzia kuhusu michezo ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Algeria na DR Congo itakayochezwa mwezi huu kwenye tarehe za kalenda ya FIFA.

Mechi dhidi ya Algeria itachezwa nchini Algeria Machi 22, 2018 na ile dhidi ya DR Congo itachezwa Machi 27, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Hata hivyo wakati Mayanga akijiandaa kuzikabili Algeria na DRC duru za ndani kutoka TFF zinasema shirikisho hilo la Soka Tanzania limeanza mikakati ya kumtafuta mwalimu mwingine atakayechukua nafasi ya kuinoa Taifa Stars.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa