Connect with us

 

Mchuano wa soka wa ligi kuu nchini Kenya kati ya watani wa jadi Gor Mahia na AFC Leopards, umeahirishwa kwa sababu za kiusalama.

Mechi hiyo inayofahamika kama Nairobi Derby au maarufu kama Mashemaji Derby, ilikuwa imepangwa kufanyika tarehe 7 mwezi Mei katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Uongozi wa AFC Leopards ambao watakuwa nyumbani, umelifahamisha Shirikisho la soka nchini humo FKF kuwa uwanja wa Afraha sio salama kwa mashabiki wa vlabu vyote viwili.

Kanuni za ligi kuu ya soka nchini humo, zinaitaka klabu mweyeji kuhakikisha kuwa inashughulikia maswala ya usalama na mambo mengine.

Kumekuwa kukushuhudiwa maelfu ya mashabiki kushuhudia mechi kati ya vlabu hivi viwili na hata wakati mwingine, hutokea makabiliano kama ilivyotokea mwaka 2010 katika uwanja wa Nyayo.

Viwanja viwili vikubwa nchini humo Kasarani na Nyayo vilivyo jijini Nairobi, vimefungwa kwa maandalizi ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN.

AFC na Gor Mahia inatarajiwa, kukutana kwa mara ya 83 katika historia ya soka nchini humo.

 

More in African Football