Connect with us

Mechi za klabu bingwa na Shirikisho kupigwa

Michuano ya soka, hatua ya mwondoano kufuzu hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika zinacheza siku ya Ijumaa na mwishoni mwa wiki hii katika viwanja mbali mbali barani Afrika.

Mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini, na zinakutanisha klabu zilizoondolewa katika michuano ya klabu bingwa na zile zilizosonga mbele katika michuano hii ya Shirikisho.

Siku ya Ijumaa, Al Ahli Benghazi itakuwa nyumbani kucheza na, Na Hussein Dey ya Algeria.

Siku ya Jumamosi, Nkana ya Zambia itamenyana na San-Pedro ya Ivory Coast, Vipers ya Uganda dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia.

African Stars ya Namibia, itachuana na Raja Casablanca ya Morocco huku Stade Malien Bamako ya Mali ikikabiliana na Petro de Luanda ya Angola.

Ratiba ya siku ya Jumapili Januari 13 2019:-

Gor Mahia vs New Star

ZESCO United vs Kaizer Chiefs

Al Hilal Omdurman vs Mukura

Otoho d’Oyo vs KCCA

Cotton Sport vs Asante Kotoko

Mechi za hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika zinachezwa mwoshi mwa wiki hii.

Siku ya Ijumaa, Januari 11 2019:

Kundi A:

Lobi Stars ya Nigeria vs Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Wydad Casablanca (Morocco) vs ASEC Mimosas (Ivory Coast)

Kundi B:

Horoya (Guinea) vs Esperance de Tunis (Tunisia)

Siku ya Jumamosi, FC Platinum (Zimbabwe) vs Orlando Pirates (Afrika Kusini)

Kundi C:

Ijumaa- Club Africain (Algeria) vs CS Constantine (Algeria)

Jumamosi- TP Mazembe (DRC) vs Ismaily (Misri)

Kundi D: Jumamosi, Januari 12 2019

Simba (Tanzania) vs JS Saoura (Algeria)

Al-Ahly (Misri) vs AS Vita Club (DRC)

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in