Connect with us

Michuano ya soka, kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon, iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita imeonesha kuwa hakuna timu ndogo katika safari ya kufuzu katika fainali hiyo.

Kundi F, ambalo lina Ghana, Kenya, Ethiopia na Sierra Leon, timu zote zina alama tatu baada ya mechi mbili.

Hii inamaanisha kuwa timu zote zimepata ushindi mechi moja na kupoteza mchuano mwingine.

Matokeo ya mwishoni mwa wiki iliyopita, Kenya iliishinda Ghana bao 1-0 jijini Nairobi huku Ethiopia ikiishinda Sierra Leon 1-0.

Kundi L, linaongozwa na Uganda ambayo haikufungana na Tanzania katika mechi muhimu iliyochezwa katika uwanja Naambole jijini Kampla.

Uganda inaongoza kundi hili kwa alama 4, huku Lesotho ikiwa na alama 2 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Cape Verde. Tanzania pia ina alama mbili katika kundi hili.

Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zina alama 4. Mechi za kundi hili zilimalizika kwa sare. Liberia waliilazimisha sare ya bao 1-1, matokeo yaliyoshuhudiwa pia katika mecho kati a Zimbabwe na Congo Brazaville.

Matokeo mengine:-

Equatorial Guinea 1 vs Sudan 0

Kusini vs 0 Mali 3
Angola 1 vs Botswana 0

eSwatini 0 vs Tunisia 2

Seychelles 0 Nigeria 3

Comoros 1 vs Cameroon 1

Msumbiji 2 vs Guinea-Bissau 2

More in Africa Cup of Nations