Connect with us

Rais wa Shiriksho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad, yupo jiini Yaounde nchini Cameroon, kukutana na rais wa nchi hiyo Paul Biya.

Ahmad, ameandama na mchezaji wa zamani wa nchi hiyo Samuel Eto’o na Makamu wa pili wa rais wa CAF Constant Omari kukutana na kiongozi huyo mkongwe.

Lengo la ziara hii ni kuzugumzia utayari wa Cameroon kuandaa mashindano ya bara Afrika mwaka 2019. Mashindano hayo, kwa mara ya kwanza, yatayashirikisha mataifa 24 badala ya 16.

Ziara hii inakuja, wakati huu uongozi wa CAF ukisema haujaridhishwa na maandalizi ya Cameroon kufanikisha mashindano haya yaliyopangwa kufanyka kati ya tarehe 15 mwezi Juni na 13 mwezi Julai mwakani.

Wiki iliyopita, CAF ilitangaza kuwa maafisa wake watakwenda nchini Cameroon mwezi Novemba kwenda kufanya thathmini ya mwisho kuhusu utayari wa nchi hiyo, hasa kuhusu hali yake ya viwanja na suala la usalama.

Maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa taifa hilo, yanaendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, jambo ambalo limewapa wasiwasi viongozi wa CAF.

Imekuwa ziara ya kwanza kwa rais Ahmad kuzuru Cameroon tangu alipomshinda Issa Hayatou, rais wa zamani wa CAF ambaye ni raia wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

More in