Connect with us

 

Mechi za mzunguko wa mwisho kutafuta timu nane zitakashiriki katika fainali ya bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 mwaka ujao nchini Zambia zinachezwa mwishoni mwa juma hili.

Michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini na mshindi baada ya mechi hizo mbili atajikatia tiketi.

Zambia imefuzu kwa sababu wao ndio watakaokuwa wenyeji wa michuano hii.

Ukanda wa CECAFA unawakilishwa na Sudan peke baada ya mataifa mengine kushindwa kusonga mbele.

Leo Misri ambao ni mabingwa mara 4 ya michuano hii watakuwa wenyeji wa Angola ambao wamewahi kushinda taji hili mara 1 jijini Cairo.

Misri ilifuzu katika hatua hii baada ya kufanikiwa kuwashinda Rwanda kwa jumla ya mabao 3 kwa 2 kupitia mikwaju ya Penalti baada ya mechi za nyumbani na ugenini.

Angola nayo, ilitinga hatua hii baada ya kuishinda Gabon mabao 3 kwa 1.

Ratiba ya Jumamosi Julai 9 2016

Gambia vs Guinea

Burkina Faso vs Mali

Senegal vs Ghana

Ratiba ya Jumamosi Julai 10 2016

Sudan vs Nigeria

Lesotho vs Afrika Kusini

Cameroon vs Libya

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili na wanashikilia rekodi ya kunyakua mataji 7 ya michuano hii mwaka 1983,1985,1987,1989,2005,2011 na 2015.

Misri wameshinda mara nne mwaka 1981,1991,2003,2013.

Ghana mara 3 mwaka 1993,1999,2009.

Cameroon (1995), Algeria (1979), Morocco(1997), Angola (2001) na Angola (2001)

Mashindano yaliyopita yalifanyika nchini Senegal mwaka 2015.

 

 

More in