Connect with us

Mfumo wa video kumsaidia mwamuzi wa kati katika mchezo wa soka kufanya maamuzi sahihi ( Video Assistant Referee) umetumiwa kwa mara ya kwanza katika mchuano wa kuwania taji la CAF Super Cup kati ya Wydad Cassablanca na TP Mazembe mwishoni mwa juma lililopita.

Shirikisho la Kimataifa linalotunga sheria za soka, linasema teknolojia hii itsasaidia waamuzi wa kati kufanya maamuzi sahihi ili kuleta usawa na haki katika mchezo wa soka.

TP Mazembe ilikuwa timu ya kwanza barani Afrika kunufaika na mfumo huu baada ya mkwaju wa penalti uliokuwa umepewa kwa Wydad Cassablanca.

Lengo kuu la mfumo huu ni kumsaidia mwamuzi kufanya maamuzi sahihi iwapo goli lilifungwa kwa haki au la. Kufanya uamuzi huu, mchezo husitishwa ili mwamuzi kuangalia bao lilivuka mstari.

Mfumo huu unasaidia pia kufanya maamuzi sahihi iwapo adhabu wa penalti umetolewa kwa usahihi.

Pamoja na hilo, unasaidia kuhakikisha kuwa uamuzi wa mchezaji anayepewa adhabu ya kuondoka uwanjani baada ya kosa kufanyika uwanjani, ni uamuzi sahihi.

Yote haya hufanyika kati ya mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wanaofuatilia mwenendo mzima wa mechi kupitia kamera maalum.

More in