Connect with us

 

Makala ya 20 fainali ya mchezo wa soka kuwania taji la bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 inaanza kutifua vumbi siku ya Jumapili nchini Zambia.

Michuano hii itachezwa katika uwanja wa taifa jijini Lusaka na ule wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, na kumalizika tarehe 12 mwezi Machi.

Mataifa yatakayoshiriki katika michuano hii ni pamoja na wenyeji Zambia, Sudan, Afrika Kusini, Senegal, Mali, Guinea, Misri na Cameroon.

Mataifa yatakayomaliza katika nne bora, yatafuzu kucheza katika michuano ya kombe la dunia nchini Korea Kusini mwezi Mei.

Mataifa yanayoshiriki katika michuano hii yamejumuisha katika makundi mawili.

Kundi la A:-Zambia, Guinea, Misri na Mali

Kundi la B:-Senegal, Sudan, Cameroon na Afrika Kusini

Mabingwa wa taji hili ni Nigeria walioshinda mwaka 2015.

Historia ya washindi wa taji hili:-

1.Nigeria imeshinda mara 7 mwaka-1983, 1985, 1987,1989,2005,2011 na 2015

2.Misri imeshinda mara 4 mwaka 1981, 1991, 2003, 2013

3.Ghana imeshinda mara 3, mwaka 1993,1999, 2009

4.Cameroon imeshinda mara 1 mwaka 1995

5.Algeria mara 1 mwaka 1979

6.Morroco mara 1 mwaka 1997

7.Angola mara 1 mwaka 2001

8.Congo mara 1 mwaka 2007

More in