Connect with us

Baraza la Mchezo wa soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ,limeahirisha michuano ya mwaka huu kati ya timu za taifa.

Michuano hii ilikuwa imepangwa kufanyika nchini Kenya katika miji ya Machakos, Kisumu na Kakamega lakini chama cha soka nchini humo FKF, kimejiondoa kwa sababu za kifedha lakini pia ratiba ngumu ya michuano ya klabu bingwa na Shirikisho iliyotangazwa na CAF.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye ameiambia tovuti ya Michezo ya soka25east kuwa, baada ya Kenya kujiandoa kuandaa mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike mwisho wa mwezi huu, imekuwa ni vigumu kumpata mwenyeji mwingine haraka.

Michuano hiyo sasa itafanyika mwezi Julai mwakani, na itatunguliwa na ile ya klabu bingwa, maarufu kama Kagame Cup mwezi Juni.

 

More in