Connect with us

Klabu ya soka ya Wydad Casablanca ya Morocco inahitaji alama moja tu katika mchuano wake dhidi ya Zesco ya Zambia kumaliza wa kwanza katika kundi A, mchuano wa mwisho wa hatua ya makundi, kufuzu nusu fainali ya mechi kutafuta ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika.

Mechi hii itachezwa siku ya Jumatano na ikiwa mabingwa hao wa mwaka 1992 watapoteza mchuano huo utakaodaliwa katika uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola watamaliza wa pili, watakutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali kutoka kundi B.

Miezi miwili iliyopita katika mchuano wa kwanza, Wydad Casablanca walipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani na wanakwenda katika mchuano huu wakiwa na saikolojia nzuri.

Klabu hii inayofunzwa na kocha wa zamani wa Real Madrid na mchezaji wa Liverpool John Toshack, wanaongoza kundi hilo kwa alama 10.

Kocha wa Zesco George Lwandamina amekuwa akisema ana imani kuwa klabu yake kufuzu lakini ana mashaka na mabeki wake.

Mchuano mwingine wa taji la klabu bingwa utakuwa ni kati ya Enyimba ya Nigeria na Sundowns ya Afrika Kusini, mchuano utakaochezwa mjini Port Port Harcourt.

 

uwanja-wa-taifa-dar

TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itachuana na Yanga FC ya Tanzania katika mchuano wa mwisho wa kundi A kufuzu katika hatua ya nusu fainali kutafuta ubingwa wa taji la Shirikisho.

Mazembe wataingia uwanjani siku ya Jumanne wakiwa na alama 10 na hata wakishindwa au kutoka sare watakuwa wamefuzu kutokana na wingi wa alama zake lakini wapinzani wao wameshaondolewa.

Medeama FC ya Ghana nayo inahitaji sare kujihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili mbele ya MO Bejaia ambao watakuwa wenyeji wao.

Klabu hii kutoka Magharibi mwa Ghana, wana alama nane, lakini wana kibarua kigumu kuhakikisha kuwa MO Bejaia ambayo ina alama 5 haiwafungi.

FUS Rabat ya Morocco nayo itakuwa mwenyeji wa Etoile du Sahel ya Tunisia, vlabu vyote ambavyo vimefuzu.

Kundi la B linaongozwa na FUS Rabat ambayo ina alama 11 huku Etoile du Sahel ikiwa na alama 10.

Kawkab Marrakech ya Morocco na Al-Ahli Tripoli ya Libya, zitamenyana katika mchuano wa mwisho siku ya Jumatano.

 

More in