Connect with us

Michuano ya klabu bingwa kupigwa wikendi hii

Michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, zinanchezwa jioni hii katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Lobi Stars vs Wydad Casablanca-Kundi A

Platinum vs Horoya-Kundi B

TP Mazembe vs Club Africain-Kundi C

Vita Club vs Saoura-Kundi D

Orlando Pirates vs ES Tunis-Kundi B

Al Ahly vs Simba-Kundi D

Siku ya Ijumaa, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, iliendelea kupata ushindi katika mechi muhimu ya kundi A, baada ya kuifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast mabaio 3-1, mjini Pretoria.

Kwa matokeo hayo, mabingwa hao wa mwaka 2016 wanaongoza kundi hili kwa alama sita.

Kundi, C zimesaliana klabu tatu tu, CS Constantine, Club Africain na TP Mazembe baada ya Ismaily ya Misri kufungiwa na Shirikisho la soka barani Afrika, kwa sababu ya mashabiki wake kuleta fujo katika mechi ya kwanza dhidi ya Club Africain mwezi uliopita, mjini Ismailia.

Fujo zilianza baada ya Club Africain kuwa kifua mble mabao 2-1.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in