Connect with us

Michuano ya Shirikisho barani Afrika wikendi hii

Michuano ya Shirikisho barani Afrika wikendi hii

Na Victor Abuso,

Michuano ya kwanza ya hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika CAF, zinachezwa mwishoni mwa juma hili katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Vlabu 16 vinashiriki katika hatua hii na vimepangwa katika makundi mawili na mshindi wa kwanza na wa pili atafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Siku ya Jumamosi, Orlando Pirates ya Afrika Kusini itamenyana na Kaloum Star ya Guinea, huku Warri Wolves ya Nigerai ikiwa nyumbani kumenyana na AC Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Siku ya Jumapili, wawakilishi watatu wa Tunisia pia watakuwa viwanjani kutafuta ushindi.

Club Africain watamenyana na Al Ahly ya Misri, Etoile du Sahle dhidi ya Raja Casablanca ya Morroco na ES Tunis watakuwa ugenini kumenyana na Hearts of Oak ya Ghana.

Wawakilishi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AS Vita Club watakuwa nyumbani jijini Kinshasa kumenyana na Stade Malien ya Mali, huku

Sanga Balende kutoka mji wa Mbujimayi wataanza mchuano wao ugenini dhidi ya Zamalek ya Misri.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in