Connect with us

Awamu ya pili ya michuano ya soka kuwani taji la kampuni ya kubashiri michezo SportPesa kati ya klabu kutoka Kenya na Tanzania itaanza siku ya Jumapili katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Mshindi atapata nafasi ya kusafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na klabu ya Everton mwezi Julai.

Klabu kutoka Kenya zitakazocheza katika michuano hiyo itakayomalizika tarehe 10 ni pamoja na Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz.

Wawakilishi kutoka Tanzania ni pamoja na Young Africans, Simba SC, Singida United na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Timu hizi zote hizi zinafadhiliwa na kampuni ya SportPesa ambayo imetoa Dola 30,000 kwa mshindi huku mshindi wa pili akipata Dola 10,000.

Ratiba kamili:-

Juni 3 2018

Kakamega Homeboyz vs Yanga

Gor Mahia vs JKU

Juni 4 2018

Kariobangi Sharks vs Simba

Juni 5 2018

AFC Leopards vs Singida United

Michuano ya hatua ya nusu fainali itachezwa tarehe 7 mwezi Juni kuelekea fainali tarehe 10.

Awamu ya kwanza ya michuano hii ilichezwa mwaka 2017 jijini Dar es salaam nchini Tanzania, na Gor Mahia ya Kenya ikaibuka mabingwa.

More in East Africa