Connect with us

Malawi na Zimbabwe zinamenyana katika mchuano muhimu wa kufuzu kucheza fainali ya vijana wasiozidi miaka 17, itakayoandaliwa nchini Tanzania mwaka 2019.

Angola ambayo ilianza vema michuano hiyo ya kufuzu baada ya kuishinda Malawi bao 1-0 katika mchuano wa kundi C, inamenyana na Zimbabwe ambayo ilifungwa na Swaziland mabao 3-2 wiki iliyopita.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Msumbiji ilifungwa na Afrika Kuisni mabao 4-1 huku Zambia ikiifunga Lesotho bao 1-0 katika mchuano mwingine muhimu wa kundi B.

Mechi za kundi hili, zitamalizika siku ya Jumanne, ambapo Lesotho itacheza na Msumbiji huku Afrika Kusini ikimenyana na Zambia.

Ratiba ya kundi A

Namibia vs Botswana

Ushelisheli vs Mauritius.

Michuano hii ya inayaleta mataifa ya Kusini mwa mataifa ya bara la Afrika COSAFA, nchini Mauriutius.

Mshindi atakeyefahamika tarehe 29 mwezi huu, atafuzu kucheza katika michuano hiyo ya Afrika.

Tanzania itakuwa miongoni mwa mataifa nane, yatakayofanyika jijini Dar es salaam mwakani.

Timu nyingine, kutoka kanda mbalimbali zitaanza kuchezwa kati ya mwezi Agosti na Septemba.

More in