Connect with us

Morocco imezindua kampeni ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia katika mchezo wa soka jijini Casablanca mwaka 2026.

Hii ni mara ya tano kwa taifa hilo la Afrika Kaskazini, kuomba wenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani baada ya kujaribu tena 1994, 1998, 2006 na 2010.

Inashindana na Canada, Mexico na Marekani ambazo zimeomba kuandaa michuano hii kwa pamoja.

Shirikisho la soka duniani FIFA, linatarajiwa kutangaza mwenyeji wa michuano hiyo tarehe 13, siku moja kabla ya kuanza kwa fainali ya mwaka huu nchini Urusi.

Mwenyekiti wa Kamati inayowasilisha maombi hayo Moulay Hafid Elalamy , Morocco inataka kuonesha dunia kuwa, ndio kitovu cha mchezo wa soka.

Hata hivyo, haijafamika Morocco imepanga kutumia viwanja gani katika michuano hiyo.

Afrika Kusini hadi sasa ndio nchi pekee ya Afrika ambayo imewahi kuwa wenyeji wa michuano hii mwaka 2010.

Kwa mara ya kwanza, mataifa 48 yatashiriki katika fainali ya kombe la dunia kutoka timu 32.

 

More in