Connect with us

Ligi kuu Tanzania bara inaanza kutifua vumbi katika viwanja mbalimbali Jumamosi hii.

Msimu mpya unaanza baada ya mchuano muhimu wa ngao ya hisani kati ya mabingwa watetezi Yanga na Simba siku ya Jumatano.

Mchuano huo, Simba walifanikiwa kuilaza Yanga kwa mabao 5 kwa 4 kupitia mikwaju ya penalti baada ya mchuano huo kukamilika kwa sare ya kutofungana.

Timu 14 kati ya 16 zinazocheza ligi kuu nchini humo zinaanza mechi zao kuanzia saa 10 jioni saa za Afrika Mashariki.

Lipuli FC,Singinda  na Njombe Mji ni timu mpya zilizopandishwa daraja katika ligi kuu.

Ratiba Jumamosi 26, 2017:-

  • Ndanda vs Azam
  • Mwadui vs Singida United
  • Mtibwa Sugar vs Stand United
  • Simba vs Ruvu Shooting
  • Kagera vs Mbao
  • Njombe Mji vs Tanzania
  • Mbeya City vs Maji Maji FC

Jumapili 27, 2017

  • Young Africans vs Lipuli

Ijumaa 01,9,2017

  • Singida United vs Mbao

Jumamosi 02,09,2017

  • Tanzania Prisons vs Maji Maji

More in African Football