Connect with us

Na Fadhili Sizya

Mtanzania Farid Mussa leo hii usiku anaweza  akaandika historia mpya ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya soka nchini Hispania(La Liga) ambapo klabu yake CD Tenerife itacheza mchezo wa pili wa mtoano kutinga katika ligi hiyo dhidi ya Getafe.

Mechi hiyo itaanza saa 4:00 Usiku katika uwanja wa nyumbani wa Getafe  Coliseum Alfonso Pérez.

Aidha mechi ya awali Tenerife walishinda bao 1-0 lililofungwa na Jorge Saenz uliochezwa kwenye uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez.

Farid Mussa alijiunga na  Tenerife akitokea Azam FC mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufuzu majaribio yake ya wiki mbili ambapo msimu wote uliopita alikuwa akitumika kikosi cha pili cha klabu hiyo.

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

More in