Connect with us

Nahodha wa Tanzania Serengeti Boys ya AFCON U-17 Gabon atimkia Israel

Nahodha wa Tanzania Serengeti Boys ya AFCON U-17 Gabon atimkia Israel

Na Mwandishi Wetu Kutoka Dar Es Salaam,

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ya Taifa Stars ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys ya mwaka 2017 iliyoshiriki michuano ya AFCON U-17 nchini Gabon Issa Makamba ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa sasa inakaribia kutimia baada ya kuripotiwa kuwa mchezaji huyo amepata timu nchini Israel na ataondoka mwisho wa wiki hii.

Issa Makamba 19, imeripotiwa kuwa anaenda Israel kufanya majaribio katika klabu ya Kiryat Shmona FC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Israel na kama akifanya vizuri atasalia katika kikosi hicho, Makamba amechukuliwa na wakala wa mnigeria James Adeniyi ambaye anaamini kuwa ana kipaji.

Hata hivyo Makamba licha ya kuwa nahodha wa Serengeti Boys ya AFCON U 2017 nchini Gabob hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mmoja kufuatia kuvunjika mguu siku mbili kabla ya kuanza kwa mashindano na Mei 21 2017 akarudishwa nyumbani Tanzania.

Makamba anaondoka baada ya kuchezea timu ya Singida United na sasa anaondoka kama mchezaji huru kwenda kujaribu bahati yake katika klabu ya Kiryat Shmona FC iliyoanzishwa 2000 na kuchukua Ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Israel msimu wa 2011/2012, kwa upande wa mafanikio ya hivi karibuni Kiryat Shmona FC imemaliza nafasi ya 10 katika Ligi Kuu ya nchini Israel msimu wa 2018/2019.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in