Connect with us

 

Mkutano Mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA, umeidhinisha pendekezo la bara Afrika kuwa na wawakilishi 9 wataofuzu katika michuano ya kombe la dunia kuanzia mwaka 2026.

Hatua hii imekuja baada ya pendekezo la rais wa Shirikisho hilo Giani Infatino kuwa mataifa 48 yashiriki katika fainali hiyo ili kutoa ushiriki wa mataifa zaidi katika michuano hiyo.

Hata hivyo, taifa la 10 la Afrika litaweza kufuzu kama litashinda michuano ya mwondoano kati ya mataifa sita.

Tangu mwaka 1998, bara la Afrika limekuwa likiwakilishwa na mataifa matano katika michuano hii.

Mbali na bara Afrika, hivi ndivyo ilivyokuwa katika mabara mengine:-

  • Asia: Nafasi 8 kutoka mataifa 4

  • Afrika: Nafasi 9 kutoka mataifa 5.

  • Kaskazini na eneo la Kati katika bara la Amerika-Nafasi 6 kutoka 3.

  • Amerika Kusini:-Nafasi sita kutoka 4.

  • Mataifa ya visiwani: Nafasi 1

  • Ulaya:Mataifa 16 kutoka mataifa 13.

More in