Connect with us

Timu ya Taifa ya Nigeria inaingia uwanjani saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika chezo wa kufa au kupona dhidi ya Argentina.

Nigeria ina alama tatu na inahitaji ushindi tu ili kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo. Argentina ya Lionel Messi pia ina alama moja na inahitaji ushindi ili kufuzu hatua hiyo huku ripoti zikisema wachezaji wamemkataa kocha George Sampaoli.

SArgentina imekutana mara nne na Nigeria katika fainali za Kombe la dunia na imeshinda mechi zote, ikiwemo ushindi wa mabao 3-2 katika hatua ya makundi fainali za mwaka 2014, nchini Brazil.

Lionel Messi haajafunga hata bao moja katika fainali hizi na atakuwa na kazi ya kuhakikisha Argentina haitoki kichwa chini katika fainali hizi.

Mchuano mwingine utakuwa baina ya Iceland na Croatia ambayo tayari imefuzu hatua ya 16 bora baada ya kushinda mechi mbili za awali.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in Swahili Stories