Connect with us

Nyota wa Tanzania Kelvin John akiri kufanya mazungumzo na KRC Genk

Nyota wa Tanzania Kelvin John akiri kufanya mazungumzo na KRC Genk

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Mtanzania Kelvin John, 16, ambaye ameonekana kuwa na uwezo mkubwa kiasi cha kujumuisha katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ya wakubwa (Taifa Stars) mara kadhaa licha ya kutopata nafasi ya kucheza, sasa ametangaza kuwa anasubiri kufikisha umri wa miaka 18 ili asajiliwe na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta.

Kelvin John akiichezea timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa miaka 17 Serengeti Boys katika michuano ya AFCON U-17 nchini Tanzania, amekuwa akionesha kiwango kikubwa kiasi cha watanzania kumfananisha uchezaji wake na Kylian Mbappe wa klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa, Kelvin John amethibitisha kuhitajika na Genk baada ya kuonekana akiwa nchini Ubelgiji akiwa na Mbwana Samatta na kufanya ziara katika uwanja wa KRC Genk na baadae kurudi Tanzania kuungana na  kikosi cha Tanzania U-20 kuelekea Uganda katika michuano ya CECAFA.

“Naweza kusema Genk wananitaka ndio lakini hawezi kunichukua kwa sasa hivi hadi nitakapofikisha miaka 18, ndio tupo katika mazungumzo hayo kwamba  nikishafikisha miaka 18 ndio wanaweza kunichukua lakini sasa hivi mimi sio mchezaji wa Genk wala sina timu yoyote nipo katika academy tu” alisema Kelvin John kutokea Jinja Uganda.

KRC Genk licha ya kumuhitaji nyota huyo inaogopa kumsajili akiwa chini ya umri wa miaka 18 kwa kuhofia kuvunja sheria za usajili za FIFA, ambazo haziruhusu mchezaji mwenye umri chini ya miaka 18 kusajiliwa na klabu iliyo zaidi ya Kiliometa 100 kutokana makazi ya familia yake yalipo (nje ya mipaka ya nchi ya mchezaji), Kwa Sasa Kelvin John yupo nchini Uganda katika michuano ya CECAFA U-20 akiichezea timu ya taifa ya Tanzania ambayo imefuzu hadi hatua ya nusu fainali kwa kuitoa Uganda U-20.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in