Connect with us
Na Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Mambo yanazidi kunnyookea mshanbuliaji wa Uganda Emanuel Okwi ambaye ameendela kung’ara katika Ligi ya Tanzania.
Mchezaji huyo amefunga Mabao matano katika mechi sita za Ligi kuu ambazo klabu yake imecheza na jukaa kileleni mwa orodha ya wafungaji.
Okwi amesema anafurahia maisha Tanzania na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji na mashabiki wa Simba.
“Kila mchezaji anataka kufunga na kuisaidia timu yake,wachezaji wenzangu wamekuwa na msaada mkubwa. Nitaendelea kujutuma na kuifungia Simba nikipata nafasi.
Mchezaji huyo amesema wachezaji wa Simba wana Kazi ya kupambana kuhakikisha timu yao inapata ubingwa msimu huu.
“Sinba ina kiu ya ubingwa hivyo wachezaji lazima tupambane sana. Tushinde taji la ligi kuu,”amesema mchezaji huyoo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Uganda

More in