Connect with us

Washambuliaji wawili wa klabu ya Simba, John Bocco na Emanuel Okwi wamepona majeraha ya mguu na wako tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba na Al Masry.

Simba itachuana na timu hiyo kutoka Misri katika mchezo unaotabiriwa kuwa na ushindani mkali baina ya timu hizo mbili, utakaochezwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Okwi na Bocco waliumia kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema wachezaji hao pamoja na Haruna Niyonzima wamefanya mazoezi na wenzao kwa ajili ya mchezo huo.

“Wote wako vizuri umebaiki uamuzi kwetu kama benchi la ufundi kuamua nani ataanza na nani atasubiri, Niyonzima ni mchezaji mzuri na urejeo wake utaongeza ushindani kikosini,”alisema Djuma.

Simba inahitaji kushinda mchezo huo kwa idadi kubwa ya mabao ili kujiweka katika maziungira mazuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Misri.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in