Connect with us
Na Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Simba itakosa huduma ya wachezaji wake wawili muhimu Emanuel Okwi na Juuko Murshid walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda ‘Uganda Cranes’.
Uganda inajiandaa na mechi ya kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Misri utakaochezwa Agosti 31 jijini Kampala.
Okwi ameanza vizuri Ligi ya Tanzania kwa kufunga Mabao manne yalimweka kileleni katika orodha ya wafungaji.
Juuko ni mchezaji muhimu katika safu ulinzi ya Simba na alikuwemo kwenye kikosi cha Uganda kilichocheza fainali za Afrika nchini Gabon mapema mwaka huu.
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema wachezaji hao wataungana na wenzao baada ya kumaliza majukumu ya timu yao ya Taifa.
“Ni wachezaji wazuri na ndio maana Basena amewaita kikosini, tuna imani watarudi mapema kujiunga na wenzao,”amesema Mayanja ambaye pia ni raia wa Uganda.
Simba inajiandaa na mchezo muhimu wa Ligi Kuu dhidi ya Azam utakaochezwa Septemba 6 kwenye Uwanja wa Uhuru.

More in