Connect with us

Ripoti: Morroco ilishinda wenyeji wa kombe la dunia 2010

Ripoti: Morroco ilishinda wenyeji wa kombe la dunia 2010

Na Victor Abuso,

Vyombo vya Habari nchini Uingereza zinaripoti kuwa, Morocco ndio iliyoshinda kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 wala sio Afrika Kusini.

Hizi ni tuhma za hivi punde za kashfa za ufisadi zinazoendelea kulikabili Shirikisho la soka duniani FIFA.

Ripoti zinasema kuwa Morocco iliishinda Afrika Kusini kwa zaidi ya kura mbili kwa mujibu wa siri iliyotolewa na aliyekuwa Mwanakamati Mkuu wa FIFA Ismail Bhamjee.

Juma lililopita,  Marekani ilidai kuwa uchunguzi wa wajajusi wa FBI umebaini kuwa Serikali ya Afrika Kusini ilitoa Dola Milioni 10 kupitia aliyekuwa Naibu rais wa FIFA Jack Warner ili kupigiwa kura na kuwa wenyeji wa kobe la dunia.

Hata hivyo, Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula  alijitokeza na kukanusha madai hayo na kusema fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuendeleza  na kusaidia soka katika mataifa ya Carrebian.

Bhamjee ananukuliwa akisema  baada ya kuhojiwa na mwahabari mmoja kuwa,  licha ya Morocco kushinda nayo pia ilitoa rushwa ya Dola Milioni 1 kwa kiogozi wa CONCACAF Jack  Warner ili kupigiwa kura.

Sakata hili la FIFA limesababisha Joseph Blatter kutangaza kuwa anajiuzulu na anatarajiwa kuitisha mkutano mkuu  ili kufanyika kwa uchaguzi mwingine, mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao.

Jack Warner aliyeondoka katika uongozi wa FIFA miaka minne iliyopita,  juma lililopita alidokeza kuwa atatoa siri ambazo amekuwa akizihifadhi kuhusu kashfa ya ufisadi katika Shirikisho hilo la soka duniani.

Sakata hili la rushwa pia limesababisha kuwepo kwa dukuduku kuhusu usafi wa Urusi kupewa nafasi ya wenyeji wa kombe la duniani mwaka 2018 pamoja na Qatar mwaka 2022.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in