Connect with us

Robert Kidiaba achaguliwa mbunge nchini DRC

Kipa wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya DRC na klabu ya TP Mazembe Robert Kidiaba, amechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la mkoa wa Katanga.

Kidiaba ambaye siku zake alipata umaarufu mkubwa kwa kutoka kwa mashabiki wa mchezo huu kwa kucheza kwa makalio, sasa ana kazi ya kuwakilisha maslahi ya watu wa eneo bunge lake katika ulingo wa kisiasa.

Wakati akicheza soka, Kidiaba mwenye umri wa miaka 42, aliichezea timu ya taifa mara 61, tangu mwaka 2002 hadi 2015.

Amekuwa pia katika klabu ya TP Mazembe tangu mwaka 2002, na baada ya kustaafu soka alikuwa kocha msaidizi hadi kuchaguliwa kwake.

Kipa huyo wa zamani alianza kujishughulisha na masuala ya siasa baada ya kustaafu kucheza soka mwaka 2015.

More in African Football