Connect with us

Wenyeji Rwanda wanachuana na Ethiopia katika mechi muhimu ya soka kusaka taji la CECAFA baina ya wanawake.

Rwanda walianza vema michuano hii baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Tanzania bao 1-0 wiki iliyopita.

Kocha Jean Baptiste Kayiranga anawaongoza wachezaji wake katika mechi hii muhimu, akitumai kuwa itapata ushindi na kusonga mbele katika mashindano haya.

Uganda ambayo ilianza vema kwa kuishinda Ethiopia mabao 2-1 inachuana na Tanzania katika mchuano mwingine siku ya Jumatatu.

Mechi ya kwanza, Uganda ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya.

Shirikisho la soka duniani FIFA, linaifadhili CECAFA, ambalo ni Baraza la Mchezo wa soka Afrika Mashariki na Kati, kufanikisha mashindnao haya yatakayomalizika tarehe 28 mwezi huu.

Mataifa yanayoshiriki ni pamoja na wenyeji Rwanda, Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia.

More in CECAFA Women's Senior Challenge