Connect with us

Baraza la Shirikisho la soka duniani FIFA, limeamua kuwa kikao chake cha nane kitafanyika jijini Kigali nchini Rwnada kati ya tarehe 25 na 26 mwezi Oktoba mwaka huu.

Uamuzi huu ulifikiwa baada ya kikao cha kwanza cha Baraza kuu la FIFA mwaka 2018  lilofanyika jijini Bogota nchini Colombia siku ya Ijumaa.

Mbali na Rwanda, jiji kuu ya Ufaransa Paris, litakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa FIFA, utakaofanyika tarehe 6 nwezi Juni mwaka 2019.

Utakuwa ni mkutano wa 69 wa FIFA, unaowaleta viongozi wote wa vyama vyote vya  soka duniani pamoja na wadau wengine wa mchezo huo.

Nchi ya Peru, imeiteuliwa  kuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 mwaka 2019.

Baraza hilo la FIFA, pia limeidhinisha matumizi ya mfumo wa teknolojia wa Video Assistant Referee kumwezesha mwamuzi kuthibitisha matukio mbalimbali uwanjani.

Mkutano Mkuu wa FIFA wa 68 utafanyika mwezi Juni mwaka huu jijini Moscow nchini Urusi, kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtafuta mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2026.

More in FIFA World Cup