Connect with us

Samatta Akanusha kunyimwa ushirikiano Aston Villa

Samatta Akanusha kunyimwa ushirikiano Aston Villa

Na mwandishi wetu akiwa Dar es Salaam,

Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ,27, amekanusha madai ya wengi kuwa alikuwa akinyimwa ushirikiano katika mchezo wa nusu fainali Carabao dhidi ya Leicester City, Samatta akiitumikia Aston Villa kwa mara ya kwanza na kutinga fainali kwa ushindi wa 2-1 (agg 3-2) mchezo uliochezwa Villa Park.

“Kwa muda niliocheza naweza linganisha na kucheza mechi mbili za Belgium, speed ya mpira wa England ni kubwa sana sio rahisi kama hauko fiti kucheza” alisema Samatta kupitia Clouds FM

Kwa upande wa wadau wa soka na mashabiki Tanzania baada ya mchezo huo walikuwa wanaamini wachezaji wa Aston Villa (aliowakuta) hawakuwa wakimpa ushirikiano yaani sapoti kwa asilimia 100, Samatta amekanusha tuhuma hizo na kutolea ufafanuzi.

“Hapana hapana mimi nakataa hicho kitu kwa sababu unajua nimetrain na timu sio zaidi ya siku 4 na mimi ni mchezaji mgeni ambaye nimetoka klabu nyingine, kwa hiyo mimi peke yangu ndio nilikuwa mchezaji mgeni katika mchezo wa jana”

“Wachezaji wote ambao walikuwa wanacheza pale walikuwa ni wachezaji ambao wameshakuwa pamoja kwa muda mrefu ni wachezaji ambao wanafahamiana, mimi nilikuwa mchezaji mgeni ni ngumu kujua movement za mchezaji mgeni katika timu, hata wakati nipo Genk mchezaji mgeni anapokuja ni lazima kupatikane muda wa ku-copy” alisema Samatta

Samatta ukiacha mtihani wa Jumamosi wa mchezo wa EPL kati ya timu yake ya Aston Villa dhidi ya AFC Bournemouth, watacheza mchezo wa fainali ya Carabao Cup Machi 1 2020 katika uwanja wa Wembley dhidi ya Man City.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in