Connect with us

Licha ya Yanga kutoka sare kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Singida United, michezo mingine pia imemzaa sare huku timu moja ikiibuka na ushindi.

Ndanda FC ikiwa kwenye Uwanja wake wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara imeibana mbavu Mtibwa Sugar kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana.

Njombe Mji nayo ikiwa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe imetoka sare ya bila kufungana na Mbao FC ya mwanza huku Kagera Sugar nayo ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons ya Mbeaya.

Mchuano wa mwisho kwa leo utakuwa baina ya Azam na Ruvu Shooting utakaoanza saa moja kamili kwa saa za Afrika Mashariki katiuka Uwanja wa Azam Complex.

Kesho kutakuwa na michezo miwili ambapo Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na mchuano mwingine utakuwa baina ya Lipuli na Stand United

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in