Connect with us

Mfaransa Sebastien Desabre huenda akatajwa kuwa kocha mkuu mpya wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes akichukua nafasi ya Sledojevic Milutin Micho ambaye alijiuzulu miezi kadhaa iliyopita.

Uganda ilikuwa ikinolewa kwa muda na Kocha mzawa Moses Basena na ambaye alikuwemo kwenye orodha ya mwisho ya makocha waliopendekezwa kuchukua nafasi ya Micho.

Makocha wengine waliokuwemo kwenye orodha hiyo ni Johnny McKinstry Ireland ya Kaskazini na Mbelgiji Emilio Ferrera.

Shirika la Habari la BBC limeripoti kuwa Desabre amewaambia waajiri wake Ismaili ya Misri kuwa atajiuzulu nafasi yake ya ukocha ili akaifundishe Timu ya Taifa ya Uganda.

Desabre hajawahi kufundisha timu ya taifa lakini amezifundisha klabu kadhaa za kaskazini mwa bara la Afrika ikiwemo Esperance ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco.

Mchakato wa kumsaka kocha atakayeifundisha Uganda Cranes uliratibiwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Zambia, Kalusha Bwalya.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in Swahili Stories