Connect with us

Swahili Stories

Sebastien Migne amuwekea kinyongo kocha wa Tanzania baada ya kufukuzwa Kenya

Sebastien Migne amuwekea kinyongo kocha wa Tanzania baada ya kufukuzwa Kenya

 Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

sho la mpira wa miguu Kenya (FKF) kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao mkuu wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Sebastien Migne ambaye kwa sasa kajiunga na timu ya taifa ya Equatorial Guinea kama kocha wao mkuu, imebainika Migne ana kinyongo na kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Etienne Ndairagije.

Mechi ya mwisho kabla ya FKF kumfuta kazi Migne ilikuwa ni mechi ya kuwania kufuzu CHAN 2020 kati ya Kenya na Tanzania, mchezo wa kwanza timu hizo zilizotoka 0-0 jijini Dar es Salaam na mchezo wa pili Agosti 4 2019 Nairobi dakika 90 zilimalizika kwa sare 0-0 katika changamoto ya mikwaju ya penati, Tanzania ikashinda kwa penati 4-1.

Kufuatia matokeo hayo FKF ikamfuta kazi Sebastien Migne siku chache baadae, baada ya kupewa kazi na Equatorial Guine mchezo wake wa kwanza tena anakutana na Taifa Stars ambayo ina kocha yule yule Ndairagije na kupoteza 2-1 baada ya mchezo Sebastien Migne alieleza kuwa hawezi hata kwenda holiday na Ndairagije ikitokea yupo Tanzania kwa madai ya kuwa wachezaji wake hawakucheza fair play.

Waandishi wa habari walipomtafuta Ndairagije kabla ya kuelekea Tunsia kwenye mchezo wake wa pili dhidi ya Libya, Etienne Ndairagije ameeleza kuwa Migne kabla hata ya mchezo huo kuanza alimfuata na kueleza kinyongo chake kuwa amesababishwa Kenya afukuzwe.

“Kuhusu fair play mimi nimemwambia sio refa, refa ndio ameruhusu mechi ichezwe kwa hiyo mimi niingie uwanjani nimwambie simamisha kama ameona kuna sababu ya kuendelea na mchezo, mimi nadhani ni shida yake binafsi kwa sababu hata kabla ya mechi kuanza alinifuata akaniambia wewe umenifukuza Kenya nikamwambia mimi sijakufukuza Kenya mimi fair nimeshinda mechi hao waliokufukuza mlikuwa na mambo yenu yeye anasema mimi nimemfukuza Kenya nashangaa kwa nini ameniambia hiyo neno” alisema Ndairagije

More in Swahili Stories