Connect with us

Senegal na Mali kutafuta mshindi wa tatu kombe la dunia kwa vijana

Senegal na Mali kutafuta mshindi wa tatu kombe la dunia kwa vijana

Na Victor Abuso,

Timu za taifa ya za soka za Senegal na Mali zitacheza Jumamosi hii kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya kombe la dunia baina ya wachezaji wasiozidi miaka 20 inayofikia tamati New Zealand.

Vijana wa Senegal waliondolewa katika hatua ya nusu fainali na Brazil siku ya Jumatano baada ya kufungwa mabao 5 kwa 0 huku Serbia wakiwashinda Mali mabao 2 kwa 1.

Fainali pia itachezwa Jumamosi kati ya Brazil na Serbia.

Nigeria na Ghana pia zililiwakisha bara la Afrika katika michuano hii ya dunia baina ya vijana duniani na kuondolewa.

Bingwa wa mwaka 2013 Ufaransa, naye aliondolewa mapema na mwaka huo Ghana walimaliza katika nafasi ya tatu.

Michuano ijayo itafanyika nchini Korea Kusini mwaka 2017.

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yalishindwa kufuzu katika michuano hii na kuyaachia mataifa ya Afrika Magharibi kutamba na kuonesha ushupavu wao wa kusakata kabumbu.

Wachambuzi wa soka wanasema soka la vijana ndilo linaloweza kusaidia mataifa ya Afrika kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya mataifa.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in