Africa Cup of Nations

Serengeti Boys kutafuta ushindi wa kwanza dhidi ya Angola

on

 

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania ya vijana wasiozidi miaka 17 inarejea tena uwanjani jioni hii katika mechi yake ya pili ya kundi B kutafuta ubingwa wa Afrika.

Serengeti Boys wanamenyana na Angola katika mchuano muhimu baada ya mechi ya kwanza kulazimisha sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Mali katika michuano inayoendelea nchini Gabon.

Mchuano huu unachezwa katika uwanja wa Amitie jijini Libreville kuanzia saa 11 na nusu jioni saa za Afrika Mashariki.

Angola nayo katika mchuano wake wa kwanza, ilitoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao 2-2 na Niger.

Kila timu katika kund hili, ina alama 1 na hivyo kuwa na uwezo wa kufuzu.

Siku ya Jumatano, Ghana ilifuzu katika hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mechi yake ya pili kwa kuwafunga wenyeji Gabon mabao 5-0.

Mechi ya kwanza, Ghana iliishinda Cameroon kwa mabao 4-0.

Guinea nayo ipo njiani kufuzu baada ya sare ya bao 1-1 na Cameroon katika mechi yake ya pili.

Mechi za mwisho za hatua ya makundi ni siku ya Jumamosi:-

Gabon vs Cameroon

Guinea vs Ghana

About Victor Abuso

You must be logged in to post a comment Login