Connect with us

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 kesho inashuka katika uwanja wa Ngozi nchini Burundi kuchuana na Somalia katika mchezo wa fainali ya michuano ya vijana ya Afrika Mashariki.

Swali muhimu ni je Serengeti Boys itaweka rekodi kwa kutwaa ubingwa huo. Bila shaka ni matamanio ya watanzania wengi kuona hilo likifikiwa.

Mwaka jana kikosi hicho kiliweka rekodi ya kufuzu kwa mara ya kwanza kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zilizofanyika nchini Gabon.

Serengeti ilifuzu hatua hiyo baada ya kuilambisha mchanga Kenya kwa mabao 2-1.

 

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in