Connect with us

Abdelilah Hafidi ameipa matumaini klabu ya Raja Casablanca ya Morocco matumaini ya kufuzu katika hatua ya fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga Enyimba ya Nigeria bao 1-0, siku ya Jumatano.

Kiungo huyo wa kati alipachika bao hilo katika dakika ya 48 ya mchuano huo, uliochezwa katika uwanja wa Aba.

Enyimba ilipoteza nafasi nyingi za kusawazisha au hata kupata ushindi.

Stanley Dimgba alipata nafasi ya kufunga kupitia mkwaju wa penalti baada ya mkwaju wa penalti kupita juu ya lango.

Mechi ya marudiano itachezwa nchini Morocco, tarehe 24 mjini Casablanca.

Nayo Vita Club ya DRC, ilijipa matumaini baada ya kulazimisha sare ya kutofungana na Al Masry ikiwa ugenini katika mjhi wa Port Said.

Mshindi wa mechi ya fainali, atajishindia Dola Milioni 1.25 na kucheza na mshindi wa taji la klabu bingwa, katika fainali ya kuwania taji la CAF Super Cup .

More in