Connect with us

Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.

Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .

Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amefahamisha mtandao huu kwamba timu yake inajiandaa kikamilifu na mchezo huo utakaocheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini Simba tunajipanga, lakini kwa sasa tunaeelekeza macho kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United,”amesema

Simba itavaana na Stand United Ijumaa katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania bara huku ikiongoza msimamo wa Ligi hiyo kwa kuwa na alama 45.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa