Connect with us

Timu ya Simba ya Dar es Salaam kesho itaanza kamepni ya kuwnaia taji la michuano ya kombe la Shirikisho kwa kuchuana na timu ya Gendarmarie ya Djibout.

Mchezo huo utaanza saa kumi kamili jioni na utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba inarudi kwenye michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya kupita misimu mitano tangu ishiriki michuano ya klabu Afrika.

Kiungo wa Simba Shiza Kichuya amesema hiyo ni hatua muhimu kwa klabu yake na anaamini itakuwa nafasi kwa wachezaji wa Simba kujitangaza.

“Huu ni mchezo muhimu kwa klabu yetu, na kila mchezaji, Simba imetumia muda mrefu kupata nafasi hii. Hivyo lazima tutumie nafasi tuliyopata kuleta mafanikio,”alisema kiungo huyo nyota.

Wachezaji wengine wanaotarajia kuibeba Simba katika mchezo wa kesho ni Emanuel Okwi, Jonas Mkude, James Kotei na John Bocco.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in