Connect with us

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa 19 inaendelea kesho kwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Stand United ya  Shinyanga.

Simba inaongoza msimamo wa Ligi hiyo baada ya kukusanya alama 45 ikifuatiwa na Yanga yenye alama 40.

Mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Mwamuzi wa katikati Florentina Zabron kutokea Dodoma ,Mwamuzi msaidizi namba moja Ferdinand Chacha wa Mwanza,mwamuzi msaidizi namba mbili Mashaka Mandemwa kutoka Mwanza,mwamuzi wa akiba Gelmina Simon wa Dar es Salaam na kamishna wa mechi anatoka Arusha,Peter Temu.

Huo utakuwa mchezo wa mwisho kwa Simba kabla ya kuchuana na Al Masry katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa