Connect with us

Simba inaingia Uwanjani jioni hii kuchuana na Ndanda katika mchezo wake wa 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku ikiwania kupata alama tatau na kuendelea kujikita kileleni.

Mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam unatazamiwa kuanza majira ya saa kumi kamili.

Simba ina alama 62 na endapo itashinda mchezo huo itafikisha alama 65 na kusaliwa na alama mbili ili kutangaza ubingwa msimu wa 2017/18.

Simba ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote katika Ligi Kuu msimu huu huku Ndanda ikihitaji alama ili kujinasua kutoka mkiani mwa Ligi hiyo.

Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema hataidharau Ndanda katika mchezo huo.

“Kila timu inatafuta alama, nasisi tunahitaji alama tatu bila kujali tunacheza na nani”amesema Lechantre.

Endelea kufuatilia mtandao wetu kwa habari zaidi kuhusu Ligi kuu Tanzania Bara

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in