Connect with us

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC huenda wakatangaza ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa wataishinda Singioda United Jumamosi.Simba inahitaji alama mbili ili iweze kufikisha alama 67 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote inayoshiriki Ligi ya Tanzania. kwa sasa ina alama 65.

Mchezo baina ya timu hizo utachezwa kwenye Uwanja wa Namfua Mkoani Singida na tayari Kocha wa Singida United Hans Pluijm ametangza kuwa ataimaliza Simba katika mchezo huo.

“Hatuna wasiwasi, Simba wana timu nzuri na wamekuwa na matokeo mazuri lakini mchezo w a mpira ni mipango na maandalizi. Sisi tumejipanga kuizuia Simba,”amesema Pluijm ambaye aliwahi kuonoa Yanga na kuipatia mataji mawili ya Ligi ya Tanzania.

Wachezaji wa Simba wamekuwa wakijinasibu kuwa wanataka kumaliza Ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja ili kusherehesha ubingwa wao.

“Tunataka ubingwa na pia tunataka kumaliza Ligi bila kupoteza mechi yoyote, tunakwenda Sindiga kusaka alama tatu,”alisema mshambuliaji Shiza Ramadhan Kichuya.Simba inanuia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kuusotea kwa misimu mitano.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in